TIMU za Yanga na Singida United sasa zitapambana Jumamosi badala ya Jumapili wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, taarifa imesema.
Mchezo huyo wa kirafiki umerudishwa nyuma kwa siku moja kwa kuwa uwanja utakaotumika kuwa na shughuli nyingine siku hiyo.
Yanga inayonolewa na Kocha Mzambia George Lwandamina itatumia mchezo huo kujaribub wachezaji wake wapya na wazamani kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Singida United timu mpya ailiyopanda Ligi Kuu inayolewa na kocha wake wazamani, Mholanzi Hans van der Pluijm .
Kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kimeweka kambi Morogoro , kitacheza mchezo wa Ngao ya Jamii, dhidi ya mahasimu, Simba ambao ni mabingwa wa kombe la Shirikisho Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa.
Comments
Post a Comment