Skip to main content

Yanga SC, Simba habaki mtu salama




Kocha wa Simba Joseph Omog (kushoto) na Yanga, George Lwandamina ambaop timu zao zitapambana Uwanja wa Taifa kuwania Ngao ya jamii.


Benedict Deodatus
TIMU kongwe na watani wa jadi, Simba na Yanga kesho wanatashuka kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika pambano la kuwania Ngao ya Jamii ambalo ni lazima mshindi apatikane, hatababaki mtu salama.

Mchezo huo utakaoanza saa 11 jioni unawakutanisha Yanga ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2016-17 dhidi ya Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho, ni wa ishara ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza Jumamosi hii katika viwanja mbalimbali.

Timu hizo zinakutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwa mara kwanza tangu mwaka 2011, ambapo Simba ilishinda mabao 2-0. Yanga ndiyo ina rekodi ya kutwaa Ngao Jamii mara nyingi zaidi.

Zinaingia uwanjani huku kila moja ikiwa imetoka kufanya usajili ambapo imeaacha baadhi ya wachezaji wake na kuwasaini wengine kwa lengo la kutaka kujiimarisha katika msimu mpya kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Timu hizi msimu huu ni kama zimebadilisha wachezaji wawili ambao wanatarajiwa kuongeza radha katika mchezo, Yanga ina mshambuliaji  Ibrahim Ajibu aliyekuwa Msimbazi kwa mara ya mwisho msimu uliopita huku Simba ina kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima aliyehamia baada ya kuichezea Yanga kwa misimu sita mfululizo.





Katika maandalizi awali Simba ilikwenda kuweka kambi Afrika Kusini ambako pia ilicheza michezo mwili ya kirafiki kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Orlando Pirates na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya mabingwa wa nchini hicho Bidvest Wits.

Iliporejea nchini, wanamsimbazi hao wanaonolewa na Kocha George Lwandamina wacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports na kushinda bao 1-0, ikaifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 kabla ya kwenda Zanzibar kuweka kambi ya  wiki moja na kucheza michezo mwili ya kirafiki ambapo ilitoka suluhu dhidi ya Mlandege na kuifunga Gulioni mabao 5-0.

Simba inatarajiwa kuwapanga katika safu ya ulinzi Aishi Manula, Salum Mbonde, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko na Method Mwanjali, huku katika kiungo mchezaji yeyote kati ya Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, James Kotei, Said Ndemla, Haruna Niyonzima  na Mwinyi Kazimoto.

Kwenye ushambuliaji wanachezaji wanaoweza kupangwa ni Shiza Kichuya ambaye msimu ulipita alikuwa na kismati cha kuifunga Yanga katika mechi mbili za Ligi Kuu na Emmanuel Okwi.

Washambuliaji wengine wa kati ni Laudit Mavugo na Juma Luizio ambao nao wanaweza kupangwa katika mchezo huo.

Wachezaji wa Simba

Kwa ujumla wachezaji wa Simba waliosajiliwa msimu huu ambao Kocha Omog anaweza kuwapanga wachezaji wowote anaowataka  ni;  Aishi Manula, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko, Salim Mbonde, Shiza Kichuya, Mzamiru  Yassin, John Bocco, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Said Mohammed, Emmanuel Mseja, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Ally Shomary, Jonas Mkude, Said Ndemla, Juma Luizio, Mwinyi Kazimoto, Paul Bukaba na Jamal Mnyate.

Wengine ni Nicholas Gyan, James Kotei, Method Mwanjali, Juuko Murshid, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Laudit Mavugo.

Yanga inayonolewa na Kocha George Lwandamina ilianza maandalizi Dar es Salaam kabla ya kwenda Morogoro ilikokaa kwa wiki moja  na kicheza mchezo dhidi ya Moro Kids na kushinda mabao 5-0 na kurejea Dar es Salaam ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United na kushinda mabao 3-2.

Walikwenda Pemba kuweka kambi ya wiki moja, wakiwa njiani, Unguja waliifunga Mlandege mabao 2-0 Uwanja wa Amaan kabla ya kwenda Pemba ambako waliifunga Jamhuri bao 1-0.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu katika mchezo wa kesho watawakosa wachezaji watatu Obrey Chirwa anayesumbuliwa na kifundo cha mguu na Geofrey Mwashiuya anayesumbuliwa na goti na mlinda mlango Beno Kakolanya ambaye pia anasumbuliwa na bega.

Wachezaji hao ni muhimu, Chirwa alicheza kwa kiwango cha juu msimu uliopita akitengeneza patina nzuri kati yake na Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Simon Msuva ambaye hatakuwepo kutokana na kusajili katika timu ya Difaa Al Jadid ya Algeria.

Katika ulinzi nyote tegemeo kwa Yanga wanaoweza kupangwa ni Youthe Rostand, Juma Abdul, Mwenyi Mngwali, Kelvin Yondan na Andrew Vincent, huku katika kiungo ni Mkongomani Kabamba Tshishimbi, Rafael Daud na Thaban Kamusoko.

Kwenye ushambuliaji wanaotarajiwa kushuka uwanjani ni Donald Ngoma, Ajib Tambwe na Antony Mathias.

Wachezaji Yanga

Kwa ujumla wachezaji wa Yanga waliofiti na yeyote anaweza kupangwa katika mchezo huo ni Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Abdallah Hajji ‘Ninja’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Pato Ngonyani , Maka Edward, Pius Buswita, Said Juma ‘Makapu’, Amissi Tambwe, Said Mussa , Matheo Anthony, Juma Mahadhi, Yussuf Mhilu.

Wengine ni Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Kevin Yondan, Andrew Vincent ‘Dante’, Papy Kabamba Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Ibrahim Ajibu, Emmanuel Martin na Raphael Daudi.

Kocha Joseph Omog ana rekodi ya kutopoteza mechi tatu dhidi ya Yanga tangu atue msimu uliopita, huku Lwandamina naye akitaka kuosha nyota yake Yanga kwa kupata ushindi wa kwanza tangu atue , baada ya kupoteza mchezo  wa mzunguko wa pili kwa kufungwa mabao 2-1.

Je, ni timu gani itaibuka na ushindi na kuwapa kicheko mashabiki wake au itakayotoka na kilio, dakika  90 ndizo zitatoa majibu.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...