Skip to main content

Wema Sepetu apanga uzinduzi babu kubwa Heaven Sent




MISS Tanzania  2006 , Wema Sepetu amepanga  kuzindua filamu yake mpya iitwayo Heaven Sent wiki ijayo na kisha kuoneshwa kwenye majumba ya sinema, Dar es Salaam na kuona moja kwa moja kwenye simu za mkononi kupitia app yake.

Uzinduzi huo amepanga kuufanya katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, kabla ya kuoneshwa katyika kumbi nyingine.

Kwa mujibu wa dondoo alizowekwa kwenye mtandao wake wa kijamii, nyota huyo amesema kuwa Filamu hiyo iko mbioni kuzinduliwa na kuwaeleza kukaa mkao wa tayari kuisubiri kwani ni nzuri.

Katika filamu hiyo ameingizaq na msanii nyota mwingine wa filamu Tanzania, Gabo Zigamba, huku mwongozaji akiwa ni Neema Ndepanya .

Nyota huyo ameandika katika mtandao wake wa Instagram:

“The Wait Is Over Ladies & Gentlemen… Iam sooo EXCITED…!!! Its Going Down… Ni ileeee Movie inayokuja ku-ShutDown kila Kitu… Tunaanza CountDown kama Hivi…. Nadhani Mnajuaga Sinaga Kazi Mbovu…. I know You all Missed Me…. Well, I missed You too…πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰ #RoadToHeaveSentPremier,”

“Kama bado huja download Wema App basi utakuwa unamiss alot… Maana ni kwenye Wema app tutapata nafasi ya kuinunua na kuiangalia huko… Lakini pia pale Mlimani City ndo tutapo enda kuiangalia kwa mara ya kwanza… Yaani Excitement yangu Haielezeki… The Countdown Continues… #RoadToHeaveSentPremier πŸ’‹πŸ’‹πŸ’‹.”

Wema ni mmoja wa wasanii wa bongo movie wanaotesa katika filamu za kibongo akiwa na sifa za kuuvaa uhusika.

Wakati huohuo, Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam leo imeitaja tena kesi inayomkabili staa huyo ya kukutwa na bangi na na kuitumia na kuiahirisha hadi Septemba 12 na 13, mwaka huu.

Mahakama, chini ya Hakimu Mkazi, Tomeas Simba imesema uamuzi wa kupokea au la kielelezo cha bangi iliyokutwa nyumbani kwa  Wema utatolewa Septemba 12.

Wema anakabiliwa na masghitaka ya kukutwa na keti mbili za bangi na msokoto mmoja, pamoja wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...