![]() |
| Wachezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake ya soka Uholanzi wakishangilia baada ya kuilaza Denmark kwa mabao 4-2 |
AMSTERDAM, Uholanzi
TIMU ya wanawake ya Uholanzi ikiwa nyumbani imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Denmark katika mchezo wa fainali.
Katika mchezo huo mshambuliaji, Vivianne Miedema aling'ara katika mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo kwa kufunga mabao mawili.
Wakati timu ya wanawake ikitwaa ubingwa huo, ile ya wanaume imekuwa ikipata shida katikatika kampeni ya kuwania fainali za Kombe la Dunia Urusi 2017.
Denmark iliowatoa mabingwa mara sita wa michuano hiyo, Ujerumani katika robo fainali, imemaliza mashindano hayo kwa masikitiko kwa kutolewa katika fainali yao ya kwanza baada ya awali kutolewa katika nusu fainali tano.

Comments
Post a Comment