Mwandishi wetu
KIWANGO kilichooneshwa na timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports kimewaacha mashabiki wa timu hiyo wakijisikia raha na kuwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri msimu huu katika mashindano ya ndani na Ligi Kuu ya Vodacom.
Wakicheza mbele ya maelfu ya wanachama, mashabiki na wadau wa soka, waliojitokeza katika maadhimisho ya Tamasha la Simba katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wacheza ji wa simba walicheza kwa uelewani mkubwa na kuwafanya mashabiki muda mwingi kuwashangilia.
Tamasha hilo majira ya saa 4 asubuhi kwa kufanyika mambo mbalimbali yakiwemo burudani kutoka kwa wasanii kama Snura, Tundaman, Juma Nature na wengine.
Kabla ya mchezo mchezaji Mohammed Hussein Zimbwe alitangazwa kuwa mchezaji bora wa klabu kwa msimu uliopita akichanguliwa na mashabiki wa timu hiyo, huku Abdallah Kibaden akitajwa akipewa tuzo ya heshima kutokana na kucheza kwa mafanikio zaidi katika klabu ya Simba.
Kivutio kingine ilikuwa ni pale mshereheshaji alipomtambulisha mlezi wa timu hiyo na mfanyabiashara maarufu Mohamed Dewji 'Mo' ambaye aliandanana na mgeni rasmi katika mchezo huo, January Makamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira kukagua timu.
Mo pia alizindua app ya Simba ambayo inamwesha mtu mwenye simu ya Smart kufungua na kupata habari mbalimbali kuhusu timu hiyo.
Vifijo na nderemo vilisikika zaidi wakati mshereheshaji, aliposema mchezaji mkongwe wa timu hiyo, Mwinyi kazimoto amekubali kwa hiari yake kuitoa jezi namba nane aliyokuwa akiivaa katika timu hiyo kwa mchezaji mpya aliyetokea Yanga, Haruna Niyonzima.
Wakati wa mchezo, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim, Kotei walikuwa kivutio kutokana na uelewano mkubwa.
Bao pekee la Simba lilifungwa na Mohammed Ibrahimu dakika ya
16 baada ya kupata pasi kutoka kwa Okwi.
Katika kipindi cha pili Niyonzima ambao walikata kiu ya mashabiki wao waliokuwa na hamu ya kuwaona uwanjani.
Niyonzima aliyeingia kipindi cha pili alikiteka 'kijiji cha Simba' kwa kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo hasa kutokana upigaji wake pasi vyenga vilivyowapa wakati mgumu walinzi wa Rayon na kutengeneza nafasi nzuri ya kufunga, kama John Bocco angekuwa makini angefunga alipobaki yeye na lango la Rayon dakika ya 72.
Bocco angekuwa makini angeweza kufunga mbao hata matatu kutokana na nafasi nzuri alizotengenezewa.
Timu iliyoaanza safu ya ulinzi ya Simba iliyoundwa na kipa Aishi Manula Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko , nahodha Method Mwanjali na Salim Mbonde 'Mndengereko' ilicheza vizuri sana.
Katika kiungo James Kotei, Mohamed Ibrahim 'Mo', Muzamir Yassin walicheza kwa uelewano wakiunganisha mabeki na washambuliaji.
Pamoja na kwamba washambuliaji Bocco, Shiza Kichuya na Okwi hawakufunga lakini walicheza vizuri.
Shomary Ally, Junas Mkude, Haruna Niyonzima, Said Ndemla, Laudit Mavugo, Nicholas Gyan na Mwinyi Kazimoto walicheza vizuri na kukonfa nyoyo na mashabiki.
Baada ya mpira kuisha mashabiki wa Simba waliondoka uwanjani wakina na furaha na kusimiliana kila walichokiona uwanjani na kuwa na matumaini timu yao kufanya vizuri katika msimu huu.
Simba: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko/Ally Shomary, Method Mwanjali, Salim Mbonde, James Kotei/Jonas Mkude, Mohamed Ibrahim/Haruna Niyonzima 'Mo', Muzamir Yassin/Said Ndemla, Bocco/Laudit Mavugo, Okwi/Nicholas Gyan na Shiza Kichuya/Mwinyi Kazimoto.

Comments
Post a Comment