Skip to main content

Vodacom yazipamba klabu Ligi Kuu


Ofisa habari wa Simba, Haji Manara (katikati) akiwa katika zulia jekundu jukwaani kuiwakilisha Yanga ambayo  haikuwa na mwakilishi wakati wa hafla fupi yakukabidhi vifaa vilivyotolewa na wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom Tanzania, Dar es Salaam jana.


Mwandishi wetu
KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa Ligi Kuu imetoa vifaa kwa klabu 16 zitakazoshiriki msimu wa 2017-18.


Kutolewa kwa vifaa hivyo jana,  ni uzinduzi rasmi  wa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 26, ikitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23, mwaka huu, kati ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu na Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho.

Hafla ya utoaji vifaa hivyo ilifanyika jana Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa klabu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi.


Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na  jezi, viatu, mipira na suti za kimichezo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Vodacom, Hisham Hendi alisema wametoa vifaa vya ubora wa hali ya juu ili kuhakikisha wachezaji wanacheza kwa ari na ushindani.

“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi tukiwa tunatakeleza matakwa ya mkataba wa udhamini  na ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki Ligi Kuu zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa Ligi,” amesema Hendi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliishukuru  Vodacom kwa kutoa vifaa hivyo na kuzitaka klabu zinazoshiriki Ligi Kuu kuzingatia na kuheshimu nembo ya mdhamini wakati wa mechi, ili kuepuka adhabu kwa kutumia kanuni na sheria .

Timu zilizopatiwa vifaa hivyo ni mabinngwa watetezi Yanga, washindi wa pili, Simba, , Kagera Sugar,  Azam FC, Mtibwa Sugar,  Stand United, Ruvu Shooting, Tanzania Prisons,  Maji Maji, Mwadui, Mbeya City, wa Mbao FC na Ndanda FC, Mji Njombe, Lipuli na Singida United.

Vodacom Imekuwa ikiidhamini Ligi Kuu ya Tanzania tangu mwaka 2008, kila msimu imekuwa ikitoa vifaa, zawadi ya fedha kwa mshindi wa kwanza hadi wa nne, mchezaji, kipa bora, timu yenye nidhamu,fedha za uendeshaji kwa TFF , kulipa waamuzi na mambo mengine.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...