![]() |
| Grace Mugabe |
KWA siku za karibuni habari zilizotawala katika vyombo vya habari n i kitendo cha Mke wa Mugabe, Garece kumtwanga mwanamitindo Gabriella Engels.
Pengine watu wengi hawajui ni kitu gani kilisababisha baba huyo kufanya tendo hilo dhidi ya mwanamke mwenzake.
Akisimulia kuhusu kipigo hicho, Gabriella ambaye ni mwanamitindo wa Afrika Kusini alisema alihisi angefariki dunia.
Katika mahojiano na Daily Mail, Gabriella alisema; "Ulikuwa ni mwisho wangu" na kwamba nilikuwa nikielekea kufa. Alikumbuka ajaribu kujikinga wakati amepiga magoti huku Bi. Mugabe akimpiga kutumia waya wa umeme hadi alipotokwa damu.
![]() |
| Gabriella Engels |
Mwanamitindo huyo alisema alihitaji kushonwa nyuzi kwenye kipaji cha uso wake kutokana na kujeruhiwa kwa kipigo.
Engels alisema: "Alinipiga vibaya, na nguvu zake zote, hakika nilidhani nitakufa," alisema na kuongeza mlinzi wa Bi. Mugabe hakumsaidia wakati alipoomba msaada.
Akijitetea Mama Mugabe alisema alipatwa na hasira wakati mwanamke huyo alipokwenda kwenye sherehe na mwanawe wa kiume Robert Jr na Chatunga Bellermine.
Engels alikana madai kwamba alikwenda kwenye sherehe watoto hao wa Mugabe na kwamba alijulishwa tu kwa Chatunga wakati mamake alipofika. Hakuwa amewahi kukutana nao kabla.
Mke huyo wa Mugabe mwenye umri wa miaka miaka 52 alitakiwa kuripoti polisi Jumanne, Agosti 15, hakufanya hivyo na kulikuwa na taarifa kuwa alirejea Zimbabwe.
Hata hivyo, polisi Afrika Kusini wamekana madai hayo.
Imesemekana sasa mke huyo wa rais atataka ulinzi wa kidiplomasia ilim asiwekwe chini ya ulinzi.


Comments
Post a Comment