![]() | ||||||||||||
| Timothy Bradley Jr (kulia) alipotwangana na Manny Pacquiao Aprili mwaka jana na kupoteza kwa pointi |
LOS ANGELES, Marekani
BONDIA Timothy Bradley Jr ambaye katika pambanop lake la mwisho Aprili mwaka jana alitwangana na Manny Pacquiao mara tatu ametangaza kujiuzulu mchezo wa ngumi.
Bradley aliyeanza kupigana katika klabu ndogo Kaskazini kwa California na kuja kuwa bondia maarufu duniani kwa kupigana ngumi kwa ngumi bila ya kurudi nyuma alitangaza uamuzi wa kujiuzulu Jumamosi.
Bradley, alitangaza kujiuzulu baada ya pambano kati ya Vasyl Lomachenko aliyeshinda dhidi ya Miguel Marriaga katika ukumbi wa Microsoft Theater Jumamosi, uamuzi ulionekana kuutoa kirahisi.
Bondia huyo miongoni mwa mapambano yake alipigana na Pacquiao mara tatu, akishinda mara moja kwa pointi kicha kupoteza mapambano mawili, la mwisho ikiwa ni Aprili mwaka jana.
"Nimepigana kwa mafanikio. Ilikuwa nzuri katika uchezaji," Bradley alisema na kuongeza kwa sasa hana ari ya kutaka kuendelea kupigana, amekusanya fedha za kutosha na yuko vizuri.
Bradley anayetimiza umri wa miaka 34, Agosti 29, mwaka huu, amestaafu nnguni akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 33 (13 KO) kupigwa mawili na kutoka sare moja, kwanza alitwaa ubingwa wa dunia wa uzani wa junior welter na welter kwa ujuma akitwaa mikanda mitano, alitengeneza mamilioni na alipoteza pambano lake la marudiano dhidi ya Manny Pacquiao ambalo lilikuwa ni pambano lake la tatu kupoteza.

Comments
Post a Comment