KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Ngao ya Jamii kati yaMabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/17, Yanga na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup), Simba 7,000 na tiketi zimeshaanza kuuzwa kwenye vituo wakala vya Selcom.
Kwa mujibu wa taatifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alfred Lucas viingilio vya mchezo huyo utakaopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Agosti 23, mwaka huu ikiwa ni ishara ya kuanza ligi vimepangwa katika makundi manne na cha chini ni sh 7,000.
Amesema VIP ‘A’ tiketi zinauzwa sh. 25,000; sehemu ya VIP ‘B’ na ‘C’ sh. 20,000; Viti vya Rangi la Chungwa sh. 10,000 na mzunguko kwa vitu vya rangi za bluu na kijani ni Sh 7,000.
Tiketi za mchezo huo ambao Yanga ndiyo timu mwenyeji zimeanza kuuzwa jana Jumanne Agosti 15, 2017 ili kuwapa fursa wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi mapema kujipeusha na usumbufu.
Katika kujiandaa na mchezo huo Yanga inayonolewa na kocha mzambia Geroge Rwandamina, imeweka kambi Pemba huku Simba iliyochini Mcameroon, Joseph Omog ikiwa Unguja, Zanzibar.

Comments
Post a Comment