Skip to main content

TFF yatoa yahimiza kukamilisha usajili Ligi Kuu, FDL, SDL




Mwandishi wetu

 SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  limelikumbusha klabu 16 zitakazoshiriki Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na la Pili kukamilisha usajili kwa mfumo wa Mtanda, TMS kabla ya siku ya mwisho.

Kwa mujibu taarifa ya TFF iliyotolewa na Ofisa habari wake, Alfred Lucas imezikumbusha kalabu kuwa zimebaki siku nne kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kwa msimu wa 2017/18.

Alisema dirisha la usajili linafungwa Agosti 6, mwaka huu na  (TFF), inatoa angalizo kwamba hakuna klabu itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kama haitapata leseni ya klabu.

Amesema baadhi ya klabu hazijachukua fomu za leseni  huku pia zilizochukua baadhi hazijarejesha na zilizorejesha zipo ambazo hazikujaza kwa usahihi.

Amesema Klabu ambayo haitapata leseni kutoka TFF, haitakuwa na nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2017/18.

Vigezo sita (6) vya mchezaji kupata leseni ambavyo ni: -

1. Kujazwa fomu ua utimamu wa afya (Medical Form).

2. Bima ya matibabu kwa mchezaji.

3. Barua ya uhamisho (Release Letter).

4. Hati ya Uhamisho wa Kimataifa kwa wachezaji wa kigeni.

5. Mikataba ya wachezaji iliyosajiliwa kwenye mfumo wa usajili TMS

6. Ada ya wachezaji wa kigeni ambayo ni Sh 2,000,000 badala ya dola 2,000 za Marekani.

Mdhamini Mkuu wa michuano hiyo yenye ushindani mkali. Vodacom wanafanya hivyo kwa mujibu wa mkataba wa udhamini.

Katika hatua nyingine, Lucas amesema kesho Alhamisi, Agosti 3, mwaka huu Kampuni ya Vodacom, itatoa vifaa vya mchezo kwa timu zote 16 za Ligi Kuu ya Vodacom.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...