BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu iliyopangwa kuchezwa mwishoni kwa kuipeleka mbele, kutokana na wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars kukusanyika na kujiandaa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana utakaofanyika Jumamosi hii kweny uwanja wa Taifa, ikiwa ni wiki ya mechi za kimataifa zinazotambuliwa na Fifa.
Katika mabadiliko hayo sasa Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea, Azam FC na Simba, Njombe Mji na Yanga Mtibwa Sugar na Mwadui FC zitacheza Septemba 6, 2017.Pia tarehe hiyo ya Septemba 6, mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Lipuli na Stand United, Singida United na Mbao, Kagera Sugar na Ruvu Shooting wakati Mbeya City na Ndanda FC .Michezo mingine mingine iliyosogezwa mbele hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na Kagera Sugar na mchezo kati ya Mbao na Tanzania Prisons utadanyika Septemba 21, mwaka huu.Pia Oktoba 11, mwaka huu, zimechi nyingne zitakuwa Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui, Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United, Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons, Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Yanga zitacheza Oktoba 12, mwaka huu.Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Yanga; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting, Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba.

Comments
Post a Comment