Skip to main content

Spurs kuivaa Real Madrid, Mabingwa Ulaya

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya

 NYON, Uswisi


RATIBA ya Ligi ya Mabingwa imepangwa, mabingwa watetezi,  Real Madrid ya Hispania watavaana na  Tottenham Hot Spur ya Uingereza  katika hatua ya makundi.Spurs imepangwa katika Kundi H na timu nyingine za Borussia Dortmund ya Ujerumani na Apoel ya Cyprus.

Mabingwa wa Scotiland Celtic wako katika kundi B linaloonekana kuwa gumu sanjari na timu za Bayern Munich, Paris St-Germain na Anderlecht.

Mabingwa wa Ligi Kuu England, Chelsea iko pamoja na Atletico Madrid, Roma na Qarabag katika Kundi C,  na Mabingwa wa Ligi ya Europa, Manchester United watakutana na Benfica, Basel  na CSKA Moscow kwenye Kundi A.

Manchester City, iliyomaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu iko Kundi F pamoja na Shakhtar Donetsk, Napoli na Feyenoord,  huku Liverpool, iliyoitoa katika hatu ya mchujo Hoffenheimimepangwa pamoja na Monaco, Spartak Moscow, Sevilla na Maribor katika Kundi E.Hatua ya makundi ataanza kupigwa Septemba 12-13, mwaka huu.



Hii ni mara ya kwanza kwa England kuwa na timu tano katika Ligi ya Mabingwa.

 Mara   ya mwisho Uingereza kuwa na timu sita katika hatu ya makundi ilikuwamsimu wa 2007-08, England ilikuwa na timu za Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal  na ziliungana na timu mbili za Scotiland za Celtic na Rangers.

 United iliyokuwa ikinolewa na Sir Alex Ferguson ilitinga fainali na kuitoa Chelsea iliyokuwa ikinolewa na Avram Grant kwa mikwaju ya  penalti.

Makundi Ligi ya MabingwaKundi A: Benfica, Manchester United, Basel, CSKA MoscowKundi B: Bayern Munich, Paris St-Germain, Anderlecht, CelticKundi C: Chelsea, Atletico Madrid, Roma, QarabagKundi D: Juventus, Barcelona, Olympiakos, SportingKundi E: Spartak Moscow, Sevilla, Liverpool, MariborKundi F: Shakhtar Donetsk, Manchester City, Napoli, FeyenoordKundi G: Monaco, Porto, Besiktas, RB LeipzigKundi H: Real Madrid, Borussia Dortmund, Tottenham, Apoel

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...