Mwandishi wetu
SIMBA imewabana mabingwa wa Ligi Kuu Afrika Kusini,Bidvest Wits kwa kutoka nayo sare bao 1-1 katima mchezo wa wake wa pili wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Sturrock Park, Afrika Kusini.
Mchezo huo ni wapili kwa Simba ambayo imeweka kambi nchini humo kujiandaa na msimu mpya wa 2017-18. Katika mchezo wa awali Jumamosi iliyopita ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Orlando Pirates.
Katika mchezo wa pili uliopigwa jana, bao la Simba lilifunwga na mlinzi mpya wa timu hiyo aliyetokea Azam FC, Erasto Nyoni dakika ya 33.
Klabu ya Simba wiki yake, katika maadhimisho Jumanne Agosti 8, mwaka huu itapambana , Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments
Post a Comment