| Kocha wa Simba Joseph Omog wapili kulia akitoka maelekezo kwa wachezaji wake. |
Mwandishi wetu
SIKU nne kabla ya kukutana, timu kongwe na zenye utani wa jadi, Simba na Yanga leo na kesho zitafanya mechi za majaribio za mwisho kabla ya kupambana Jumatano katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwennye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya kuzindua mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Timu hizo mbili zimeweka kambi Zanzibar kujiandaa kwa pambano lao, Yanga iliyokuwa ya kwanza kwenda huko iko pemba huku Simba ikiwa Unguja.
| Wachezaji wa Yanga wakinyoosha viungo |
Katika michezo wao ya kujipima nguvu ya mwisho Yanga iliifunga mlandege mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan huku Simba ikitoka suluhu na timu hiyo katika mchezo mwingine.
Katika kujipima nguvu Simba leo itapambana na Gulioni kwenye Uwanja wa Amaan, mchezo ambao unatarajiwa kurushwa na kituo cha televisheni cha Azam.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga watashuka Uwanja wa Gombani uliopo Pemba kupambana na Jamhuri .
Mechi zote zitarushwa kituo cha televisheni cha Azam.
Comments
Post a Comment