TIMU ya Simba baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii Jumatano iliyopita, imewapa furaha furaha tena mashabiki wake kwa kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 Ruvu Shooting katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania.
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Uhuru maarufu kama Shamba la Bibi mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi alikuwa mwiba mchungu kwa Shooting yenye maskani yake mkoa wa Pwani kwa kufunga mabao manne, huku Shiza Kichuya, Juma Luizio na Erasto Nyoni kila mmoja akifunga bao bao moja.
Comments
Post a Comment