![]() |
| Baadhi ya wachezaji wa Sumba walipokuwa wakiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo. |
KIKOSI cha Simba, kimewasili mchana jijini Dar es Salaam kwa ndege, kikitokea Unguja walikoweka kamba kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, utakaopigwa keshokutwa Uwanja wa Taifa.
Yanga ndiyo iliwahi kwenda Zanzibar kisha akienda kuweka kambi Pemba, siku ya pili Simba ndiyo ilitua Unguja na kufanya maandalizi na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Mlandege (0-0_ kicha shidi ya Gulioni mabao 5-0).
Simba imetua kwa ndege, Yanga wanatarajiwa kurejea jijini kesho saa nane mchana wakitokea Pemba ambapo nao waliweka kambi ya takribani wiki moja na nusu kujiandaa na mchezo huo.

Comments
Post a Comment