Mwandishi wetu
KINYANG'ANYIRO cha Ligi Kuu ya Tanza kinaanza kesho kwa kupigwa mechi saba ambazo zitakutanisha timu 14, Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Simba wakiaanza nyumbani uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuchuana na Ruvu Shooting, huku mabingwa wa tetezi Yanga ikicheza keshokutwa kwenye uwanja huo.
Kwa mujibu wa ratiba Ndanda itaanza kucheza itaikaribisha Azam kweney uwanja wa Nang'wanda Sijaona, Mwadui itachuana na timu mpya katika ligi hiyo, Singida united kwenye uwanja wake wa Mwadui Complex Shinyanga na Kagera Sugar iliyomaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita itachuana na Mbao kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Timu nyingine mpya iliyopanda daraja, Njombe Mji itakuwa nyumbani kuvaana na Tanzania Prisons huku Mbeya City itapambana na Majimaji kwenye Uwanja wa Sokoine.
Uzinduzi wa Ligi hiyo ulifanyika Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa Mabingwa wa Ligi Kuu 2016-17 kupambana na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Simba walioibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 5-4.
Ratiba kamili ya mzunguko wa kwanza ni kama ifuatavyo:



Comments
Post a Comment