Skip to main content

Simba ilivyotwaa Ngao ya Jamii mbele ya Yanga



Wachezaji wa  Simba wakishangilia baada ya kupewa Ngao ya Jamii kwa kuilaza yanga kwa mikwaju ya penalti 5-4 lwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.

SIMBA imeanza msimu kwa neema kwa kutwaa Ngao ya Jamii  baada ya kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalti  5-4 dhidi ya watano wao wa jaji Yanga  kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga awali ndiyo ilikuwa ikishikilia ngao hiyo baada ya mwaka jana kuifunga Azam FC bao 1-0.

Katika mchezo huo uliopigwa jana uliohudhuriwa na mashabiki wote timu zote zilicheza kwa kujihami kukwepa kufungwa  na kufanya mashambulizi ya kushitukiza, zikajikuta zikimalzia dakika 90 bila ya mshindi kupatikana.

Kikosi cha Yanga kilichoanza kutoka kulia mstali wa mbele ni Juma Abdul, Kelvin Yondani Youthe Rostand, Rmmanuel Martin, Gadiel Michael. Mstari wa nyuma  ni Ibrahimu Ajibu, Raphael Daudi, Donald Ngoma, Andrew Vincent ‘Dante’, Papy Tshishimbi na Thabani Kamusoko.

Kiungo mshambuliaji wa Simba aliyetokea benchi, Mohamed Ibrahim 'Mo' ndiye aliwapa raha  mashabiki wa Simba kwa kufunga penalti ya ushindi  ikiwa ni ya sita baada ya kufungana mabao 4-4 hadi zilipoisha penalti tano.

Yanga ilikuwa ya kwanza kupiga penalti, Kelvin Yondan alikosa kwa mkwaju wake kuokolewa na  Aishi Manula, huku Papy Tshishimbi, Thaban Kamusoko,, Ibrahimu Ajibu na Donald Ngoma wakifunga wakati penalti ya Juma Mahadhi akikosa ya sita kwa kupaisha juu. 


Kikosi cha Simba kilichoilaza Yanga. Mstari wa mbele kuanzia kushoto ni Shiza Kichuya,
Aishi Manula,,  Mzamiru Yassin, Ally Shomari. Nyuma ni Laudit Mavugo, Salim  Mbonde, Erasto nyoni , James Kotei, Emmanuel Okwi  na Method Mwanjali.

Wakati Mchezaji Bora wa Ligi Msimu wa 2016-17 na Mchezaji Bora wa  Simba, Mohammed Hussein Zimbwe akikosa penalti ya tano ambayo ingeipa ushindi timu yake, baada ya kuokolewa na mlinda mlango wa Yanga, Rostand Youthe, wengine waliofunga ni Method Mwanjali, Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima.


Kocha wa Yanga, Geoge Lwandamina ameshindwa kuweka rekodi ya ushindi mbele ya Simba, ilipoteza katika Kombe la Mapinduzi Zanzibar, kutoka suluhu na kufungwa mabao 2-1 katika Ligi Kuu msimu uliopita.

Yanga ikicheza bila ya kuwa na wachezaji wake waliokuwa tegemeo msimu uliopita, Simon Msuva (aliyekwenda kucheza soka ya kulipwa Morocco), Obrey Chirwa (majeruhi),  raia wa Mali, Vicent Bossou (aliyemaliza mkataba) na Haruna Niyonzima ( aliyehamia Simba) ilicheza kwa uelewano na kuwabana Simba ambao walionekana kama wangeibuka na ushindi katika dakika 90 za mchezo.

Hadi mwisho wa mchezo ni mashabiki wa Simba walioondoka kwa shangwe uwanjani baada ya kutwaa Ngao ya Jamii, timu hizo zitakutana Oktoba 14, mwaka huu katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania.

Yanga: Youthe Rostand, Juma Abdul/Hassan Kessy, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kevin Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Raphael Daudi/Juma Mahadhi, Thabani Kamusoko, Ibrahim Ajibu, Donald Ngoma na Emmanuel Martin.

Simba:  Aishi Manula, Ally Shomari, Erasto Nyoni/Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salim Mbonde, Method Mwanjale, James Kotei, Shiza Kichuya, Mzamiri Yassin/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Laudit Mavugo/Juma Luizio, Emanuel Okwi na Haruna Niyonzima.



Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...