![]() |
| Zuwena Mohamed a.k.a Shilole |
Mwandishi wetu
MWANAMUZIKI Zuwena Mohamed maarufu kwa jina la Shilole au Shishi baby) ameeleza maana ya wimbo wake mpya wa Kigoli.
Akizungumza Dar es Salaam leo amesema neno Kigoli alilolitumia katika wimbo wake linamaanisha mwanamke mpambanaji mtafutaji na si kama watu wengi wanavyofikiria kuwa ni mwanamke ambaye bado ni bikira.
Amesema kwa kuwa yeye ni mpambanaji, akiwa na kipaji cha kuingiza, kuimba na kufanya biashara ikiwemo cha kuuza chakula anajiona ni Kigoli.
Akizungumza katika mahojiano na kipindi cha televisheni cha 360, Shilole amesema wimbo anashukuru wimbo wake wa Kigoli ambao umetoka sambamba video yake umepokewa na mashabiki vizuri.
Amesema uchezaji wake katika video hiyo (mauno), unaonesha muziki wa kiafrika ikiwemo kabila lake la wanyamwezi.
Shilole amesema yeye hasiki kwa namna yoyote kutokana na kuvunjika kwa ndoa ya aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda.
Amesema uwezekano wa kurudiana na Mziwanda haupo kwa kuwa kipindi chao cha mapenzi kilishaisha na akapata mwingine na yeye kwa sasa ana mtu wake.
Amesema kwenye mwili wake kuna michoro ya tatoo 18, amekuwa akichorwa maelekezo yake, kila mmoja una maana yake yamo hata majina mawili ya wanawe, kwa kuwepo kwenye mwili wake ni kama maua ndani ya bustani.
Amesema amepata nafasi ya kushiriki maonesho ya Fiesta hatasita kwa kuwa amefaidika nayo kiasi cha kuweza kujenga nyumba, anaamini yeye nyimbo zake zinachezeka na mashabiki hupagawa anakuwa jukwaani


Comments
Post a Comment