Skip to main content

Shija aahidi kuleta mapinduzi ya soka Tanzania



Shija Richard

MGOMBEA Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mwenye umri mdogo zaidi miongoni mwa mwa wagombe wa nafasi hiyo, Shija Richard Shija  amepanga kuleta mapinduzi makubwa katika mchezo huo nchini kama atachanguliwa katika nafasi hiyo nyeti.

Katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, wakati akifanya kampeni ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Jumamosi ya Agosti 12 mkoani Dodoma Shija alisema kwamba soka ya Tanzania ili kuwa juu, inahitaji kuwa na mipango ya muda mfupi na muda mrefu ambayo yeye anayo.

Hii ni mipango ya Shija aliyoiainisha katika taarifa yake.

 “Uhalisia ni kuwa kwa wale watakaochaguliwa watakuwa na fursa ya kuongoza kwa
miaka minne. Siku hizi hakuna biashara ya mapinduzi kwenye mpira wa miguu.

Ni dhahiri kuwa kila aliyeingia kwenye uchaguzi ana ajenda hata kama anagombea
nafasi ya ujumbe. Ajenda inabebwa na malengo ya mgombea kama alivyoyaanisha au
kuyataja katika fomu yake ya kuomba uteuzi.
Hivyo wagombea wana wajibu wa kutangaza ajenda zao mbele ya wapiga kura ambao
ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.
Mpira wa miguu ndani ya uwanja na nje ya uwanja (uongozi) umetoka wapi na sasa uko wapi. Ikiwa kila mgombea amelifanyia utafiti hilo, basi atakuwa na ajenda
iliyomsukuma na yeye kuingia kuchangia ustawi na maendeleo ya mpira wa miguu nchini katika ngazi hiyo ya juu.

Shijja Richard akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam

Ajenda ya mgombea haiwezi kunakshiwa kwa kusema fulani hakuwa kiongozi mzuri, fulani hana uzoefu wala fulani hivi, bali itatiwa nakshi na maelezo ya kwa nini huu
ndiyo wakati wake na njia zipi zitatumika kuitekeleza.
Katika uongozi wangu nitaweka Dira (Vision) ili kila mwanafamilia ya mpira aweze
kutambua uelekeo wetu kama taasisi. Pia Dira hiyo itaenda sambamba na dhima
(Mission).
Naamini kampeni za matusi, kashfa, kejeli hazina nafasi katika uchaguzi wa TFF
ambayo ni taasisi inayoheshimika- kubwa ikiwa inasimamia mchezo ambao si tu
unaongozwa kwa kupendwa Tanzania bali duniani kote kwa ujumla.
KAMPENI ZA UCHAGUZI NAFASI YA RAIS WA TFF
Kampeni zangu zitajikita zaidi kutangaza sera na mikakati niliyonayo nitakapopewa
fursa ya kuiongoza TFF.
Rais wa TFF ni nafasi kubwa, ndiye kiongozi Mkuu wa shirikisho hilo. Pia ndiye
kiongozi wa Kamati ya Utendaji inayoshughulika na masuala ya kisera ya taasisi hiyo
ya mpira nchini.
Masuala ya kiutendaji yanashughulikuwa na Katibu Mkuu wa TFF. Kutokana na ukweli
huo, kampeni zangu zitajikita zaidi kutangaza mambo ya kisera ya TFF, badala ya
masuala ya kiutendaji.
DIRA
Kutengeneza fursa, uwezeshaji na furaha kupitia mpira wa miguu
Dhima
i. Kutengeneza na kusimamia miundombinu ya kutambua na kuendeleza vipaji vya
wachezaji
ii. Kuboresha mafunzo kwa ajili ya kupata makocha, madaktari wa michezo na
waamuzi na watawala wa michezo kwa kiwango kikubwa cha ubora
iii. Kusimamia utawala bora katika utendaji wa taasisi za michezo mkazo zaidi
ukiwa wanachama wa TFF
iv. Kusimamia vyombo vya kitaasisi vilivyopo ili viweze kufanya kazi kwa uhuru
bila kuingiliwa.
UFAFANUZI;
Mafanikio katika mpira sio jambo la kufumba na kufumbua macho. Yanakuja baada
ya kuweka misingi imara itakayosaidia kuchezeka kwa mpira.
Misingi hii huchukua muda mrefu kuijenga na kuikamilisha. Nchini Tanzania
changamoto kubwa naiona katika mfumo rasmi wa kutambua na kuendeleza
wachezaji pamoja na heshima ya TFF kama taasisi makini inayosimamia mpira.
Kutatua changamoto hizo kunaweza kuchukua miaka mingi, hivyo tunahitaji mpango
endelevu, kama ilivyo katika utawala hapa nchini ambapo kuna Vision 2025 iliyoanza
mwaka 1995.
Kwa kuzingatia hilo, nimegawa sera zangu katika mipango ya muda mrefu na mfupi.
Mipango ya muda mfupi ni ile nitakayoitekeleza ndani ya utawala wangu, wakati ile ya
muda mrefu itakuwa mwendelezo wa Vision ya miaka 20 ijayo katika mpira wa miguu
hapa nchini.
A. MIPANGO YA MUDA MREFU
1. KUTAMBUA VIPAJI
Mchezaji wa mpira anatakiwa kuandaliwa kuanzia umri wa miaka 6. Katika umri huo
watoto wa kitanzania wanakuwa shuleni.
Kunatakiwa kuwapo mfumo rasmi wa kuwatambua wachezaji wakiwa wadogo. Kwa
kuwa michezo imerudi shuleni tutaweka mpango endelevu wa kutoa mafunzo kwa
walimu wa michezo shuleni, ili waweze kuwapa wanafunzi mafunzo stahili kwa umri
wao.
Pia mpango huo utaelezea mfumo rasmi ambapo walimu hawa watakuwa wanaripoti
kwa mratibu wa mpira wa miguu wa mkoa. Huyu atakuwa ni mwajiriwa wa TFF.
Ataripoti kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Makao Makuu.
Atakuwa akiwasimamia walimu wa michezo shuleni, akiwa na lengo la kutambua
wanafunzi wenye vipaji na atahifadhi kumbukumbu na takwimu kuhusu wachezaji
hawa.
Pia atatoa mapendekezo ya wanafunzi wanaostahili kupelekwa shule maalumu za
vipaji vya mpira wa miguu ‘sports academy’.
2. KUENDELEZA VIPAJI
Baada ya kuwa na mfumo wa kutambua vipaji, sasa vipaji hivyo vinatakiwa
kuendelezwa. Hapo ndipo tunapohitaji uwepo wa shule maalumu za vipaji vya
michezo.
Wanafunzi wenye vipaji vya mpira wa miguu wanatakiwa kuwekwa kwenye shule
maalumu ili kupata muda wa kutosha kuendeleza vipaji vyao, lakini pia kuwa na
miundombinu rafiki karibu nao.
Kama taasisi tutaweka malengo ya kuwa na sports academy katika kanda sita. Kanda
ya Kati, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Ziwa
na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Katika kipindi cha miaka 20 ijayo huu ndio uwe mkakati wetu. Lakini katika kipindi
changu cha uongozi yaani miaka minne, nitahakikisha shule moja ya aina hiyo
inajengwa kanda ya Kati Dodoma kwa ajili ya kuvipokea vipaji hivyo na kuviendeleza.
Nitaalika serikali, mashirika ya umma na taasisi za watu binafsi kujenga shule hizo
kwenye Kanda ambazo tumeziainisha ili kuweza kuwa na mfumo uliosambaa kwa
usawa nchi nzima katika kuendeleza vipaji hivi.
3. KUIMARISHA TFF KITAASISI
Tunahitaji kuwa na taasisi imara na yenye kuheshimika machoni pa Watanzania na
ulimwengu kwa ujumla, ili kushawishi wadau kujitoa katika kufadhili na kuendeleza
michezo.
Uongozi wa kaka yangu LeodegarTenga ulifanikiwa kujenga misingi ya kitaasisi ndani
ya TFF.
Kuendeleza msingi mzuri wa kitaasisi uliopo kwa kuhakikisha unafanya kazi
inavyotakiwa. Mpira unabeba maslahi ya Watanzania wengi. Taasisi inayoongoza
mpira inatakiwa kuongozwa kwa umakini na ufanisi mkubwa.
B. MIPANGO YA MUDA MFUPI
Katika kipindi changu cha miaka minne nimekusudia kufanya mambo muhimu kama
ifuatavyo:-
1. KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA AZIMIO LA BAGAMOYO
Kusimamia utekelezaji wa Azimio la Bagamoyo katika maeneo makuu manne,
*Taasisi za mpira na Utawala, Ufundi, Upatikanaji wa vifaa bora na Uhuru wa
vyombo vya kikatiba.
UTEKELEZAJI: -Nitasimamia kwa nguvu zote Road Map ya utekelezaji wa Azimio la
Bagamoyo kwa kusisitiza masharti kwa klabu na vyama vya soka yatakayohakikisha
Azimio la Bagamoyo linatekelezwa kwa vitendo,".

SHIJA RICHARD SHIJA, MGOMBEA URAIS WA TFF, DAMU MPYA, MTAZAMO MPYA, MABADILIKO NI SASA.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...