![]() |
| Maria Sharapova akifurahi baada ya kumshinda Simona Halep. |
NEW YORK, Marekani
MARIA Sharapova amerejea kwa kishindo katika mashindano ya tenisi makubwa ya kila mwaka (Grand Slam) kwa kumtoa mchezaji namba mbili kwa ubora duniani, Simona Halep katika michuano ya Marekani.
Mchezaji huyo raia wa Urusi alishinda seti 2-1 akipata alama 6-4 4-6 6-3 katika pambano ambalo lilihudhuriwa na mashabiki 24,000 mjini New York.
Sharapova mwenye umri wa miaka 30, amecheza mechi ya kwanza ya mashindano ya Grand Slam baada ya kutumikia adhabu yake yake ya kufungiwa kwa miezi 15.
![]() |
| Maria Sharapova (kushoto0 akipena mkono na Simona Halep. |
Bingwa huyo wa 2006 na mchezaji bora namba moja duniani alilazimika kucheza mapambano ya kujiweka sawa kabla ya kuruhusiwa kucheza mashindano hayo makubwa na sasa yuko katika nafasi ya 146 kwa ubora.
Sharapova alitumia muda wa saa mbili na dakika 44, Sharapova kabla ya kuibuka na ushindi katika pambano hilo, akimshinda Halep licha ya kufanya makosa 64.
Sharapova anasonga mbele na kesho atapambana na Timea Babos wa Hungary , ambaye katika ubora duniani yuko namba 59.
Katika mchezo mwingine, Venus Williams aliibuka na ushindi dhidi ya Viktoria Kuzmova ambaye ni yuko katika 135 kwa ubora duniani kwea alama 6-3 3-6 6-2.
Naye Caroline Wozniacki alimshinda Mihaela Buzarnescu kwa seti 2-1 akipata alama 6-1 7-5.
Wozniacki atapambana na Ekaterina Makarova katika mchezo wake unaofuata.


Comments
Post a Comment