Caster Semenya
LONDON, Uingereza
MOJA kati ya vivutio mashindano ya riadha ya Dunia London yatakatoanza Ijumaa wiki hii ni mwanariadha Caster Semenya ambaye alizua utata kuhusu jinsi yake kutokana na kukimbia kwa kasi kama mwanaume.
Katika mashindano hayo, Semenya amesema anataka kutwaa medali mbili za dhahabu katika mbio za wanawake meta 800 na meta1,500.
Nyota huyo wa Afrika kusini mwenye umri wa miaka 26 anapewa nafasi kubwa ya kutwaa medali katika mbio za meta 800, akitaka kutwaa ubingwa wake wa tatu akiongezea medali ya dhahabu ya Olimpiki aliyotwaa Rio de Janeiro mwaka jana, na anatashiriki kwa mara ya kwanza mbio za meta 1500 katika mashindano ya kimataifa akiwa na nia ya kutwaa medali ya dhahabu.
Mashindano ya Dunia ya Riadha yanatarajia kuanza mjini London, Uingereza kuanzia 4 hadi 13 mwaka huu, baadhi ya mashabiki wanaona Semenya kwa kuwa na homoni nyingi za kiume 'testosterone' inampatia faida dhidi ya wapinzani wake.
Semenya mwezi uliopita alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Afrika Kusini, SuperSport na kusema hapendi kuulizwa swali mara kwa mara kuhusu jinsi yake na kwamba homoni alizonazo zinamsaidia kupata ushindi.
'' Sielewi wakati unaposema nina faida kwa kuwa mimi ni mwanamke, ninapokojoa ninakojoa kama mwanamke. Sikuelewi unaposema mimi ni mwanaume au nina sauti nene. Ninajua kuwa mimi ni mwanamke kwa hiyo hakuna swali kwangu.''
Alisema baadhi ya waandishi wamekuwa wakiuliza swali hilo kwa lengo la kumtia hasira, lakini yeye amejifunza jinsi ya kujibu na analigeuza suala lake kuwa chanya anashukuru familia yake inamuunga mkono.
Baada ya Semenya kutwaa ubingwa wa dunia 2009 akiwa na umri wa miaka 19, ilizua mjadala na kusababisha kuhakikiwa jinsi yake na kupimwa ambapo ilionekana ana homoni za kiume zinazofanya awe na nguvu zaidi kuliko wapinzani wake.
Baada ya kusimamishwa kushiriki riadha kwa wanawake miaka mwili kutokana na suala la homoni zake, Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) iliingia kati suala hilo na kumruhusu Semenya kurejea kwenye mchezo mwaka 2015.
Katika mbio za maandalizi za Diamond League Monaco alitumia muda wa dakika 1:55.27 meta 800 ukiwa ni muda wa kasi zaidi katika kipindi cha miaka 10, alikaribia kuivunja rekodi ya Jarmila Kratochvilova wa Czech ya mwaka 1983.
Semenya ameamua kushiriki mbio za meta 1,500 London, anajiandaa kupambana na
Genzebe Dibaba kutoka Ethiopia.

Comments
Post a Comment