![]() |
| Clement Sanga |
Mwandishi wetu
KAIMU mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na Ahmed Yahya watachuna kuwania uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 15 mwaka huu Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyotolewa jana, majina nane ya wagombea yamepita katika mchujo wa awali kuwania nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi.
![]() |
| Ahmed Yahya atatetea nafazi ya Mwenyekiti Bodi ya Ligi Tanzania. |
Imeongeza James Bwire na Almas Kasongo wamepitishwa kuwania ujumbe wakitokea klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu hakuthibitishwa na klabu yake.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Edga Chubura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.
Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika.
Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.
Uchaguzi huo wa kamati hiyo utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam na unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.


Comments
Post a Comment