Skip to main content

Ruvu Shooting yalipua mitambo Yang







Mwandishi Wetu
RUVU Shooting imelipua mitambo ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Yanga kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kujipima nguvu (kujaribu mitambo), Ruvu ilipata bao lao la zawadi  dakika ya 22 baada ya mlinzi mpya wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu  'Ninja' kujifunga kwa kupiga mpira kichwa akiwa katika harakati za kuokoa krosi iliyopigwa na mshambuliaji wa Shooting, Shala Juma.

Juma baada ya kuwatambuka wachezaji wawili wa Yanga alipiga krosi kali, Ninja aliruka kwa lengo la kutaka kutoa nje,lakini mpira uliongeza kasi na kuelekea langoni kwake na kupishana na mlinda mlango mpya wa Yanga aliyekuwa akichezea timu ya Serengeti Boys, Ramadhan Kabwili, kabla ya kutinga wavuni.

Comments