![]() |
| Cristiano Ronaldo na Lieke Martens |
NYON, Uswisi
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldoametajwa kuwa mchezaji bora wa Mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa) akimshinda, Lionel Messi na mlinda mlango wa Juventus, Gianluigi Buffon .
Ronaldo (32), aliisaidia Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo na kumalzia kama mfungaji bora wa mashindano hayo akipachika mabao12.
Mreno huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa ameweka rekodi ya kutwaa tuzo hiyo mara tatu, akimzidi Messi mara moja.
Kwa wanawake mchezaji wa Barcelona ambaye ni raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24, Lieke Martens alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa shirikisho hilo.
Martens aliisaidia nchi yake kutwaa ubingwa wa Ulaya katika majira haya ya joto na kutajwa mchezaji bora wa mashindano hayo.
Alimshinda mshambuliaji wa Wolfsburg,ernille Harder na kiungo wa Lyon, Dzsenifer Marozsan .
Tuzo nyingine ijulikanayo kama 'President's Award' imetwaliwa na Francesco Totti, aliyestaafu soka Julai baada ya kuichezea timu ya Roma kwa miaka 24, ni mchezaji aliyeichezea timu moja tu.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 40 kwa sasa amepewa wadhifa wa Mkurugenzi wa klabu hiyo.
Tuzo nyingine zilizotolewa kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa 2016-17
Mlinda mlango bora : Gianluigi Buffon
Mlinzi bora:Sergio Ramos
Kiungo Bora: Luka Modric
Mshambuliaji Bora:Cristiano Ronaldo

Comments
Post a Comment