Skip to main content

Ronaldo ataka kuhama Madrid, kurejea England



Cristiano Ronaldo  alipokuwa mahakamani nchini Hispania Jumatatu iliyopita.

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI nyota Real Madrid, Cristiano Ronaldo  amekiri kuwa anataka kuondoka katika timu hiyo mabingwa wa Ligi Kuu ya Hispania na Ligi ya Mabingwa Ulaya na kurejea tena England.

Nyota huyo ametoa kauli hiyo mufa mfupi kabla ya timu yake kupambana na United katika mechi ya kuwania Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya  UEFA (UEFA Super Cup).

Madridi ni mabingwa  wa Ulaya huku United ni bingwa wa Ligi ya Europa.

Radio Cadena Ser ya  Hispania imesema Ronaldo alisema hayo wiki hii  katika mahakama kuu ya Hispania wakati alipokwenda kusikiliza kesi inayomkabili ya tuhuma za kukwepa kodi kiasi cha euro milioni 14.7 (zaidi ya sh. bilioni 38.7) kutokana na haki zake za matumizi ya picha zake kibiashara.

Kesi yake ilisikilizwa kwa faragha mbele ya jaji Monica Gomez Ferrer Jumatatu na haikuwa kitu cha kushangaza habari za kesi hiyo kuvuja kwa vyombo vya habari kutoka na umaarufu wa Ronaldo.

Cadena Ser imeripoti kuwa Ronaldo alimwambia jaji : ' Sikuwa na matatizo kama haya nilipokuwa England… Ndiyo maana ninapenda kurejea  England.’

Ronaldo ameonekana kukasirika kutokana na kutuhumiwa kukwepa kodi na gazeti la ‘A Bola’ la Ureno limesema kuwa ameamua ataondoka Hispania kutokana na suala hilo.

Huku timu ya  PSG  ikimnyakua Neymar na Manchester United imekuwa ikihisi inaweza kumsaini tena mchezaji wao wa zamani Ronaldo.

Baada ya kusikilizwa shauri lake kwa dakika 90 katikati ya wiki, Ronaldo alionekana kuwa na wazo la kuondoka katika majira haya ya joto bado liko kichwani mwake.

Real Madrid iko tayari kuuza mmoja kati ya washambuliaji wake watatu, Karim Benzema, Ronaldo na Gareth Bale katika majira haya ya joto na ili kutoa nafasi kwa Kylian Mbappe (18) ambaye thamani yake inatajwa kuwa euro milioni 180 (zaidi ya sh. bilioni 474), ambaye amesema hataki kuhamia katika timu ambayo itamweka benchi.
 want to come only to sit on the bench.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...