![]() |
| Cristiano Ronaldo |
MADRID, Hispania
ADHABU ya kufungiwa mechi tano aliyopata, Cristiano Ronaldo kutokana na kukosa la kumsukuma refa wakati wa mchezo wa kuwania Kombe la Supercopa de Espana kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona itaendelea, baada ya rufaa aliyokata kushindwa.
Ronaldo na Madrid walikata rufaa kwa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ya Hispania (TAD), ambayo imekazia uamuzi au adhabu iliyotolewa awali.
Katika mchezo wa awali, Mreno huyo alitokea benchi na kufunga bao zuri kwenye Uwanja wa Camp Nou, wakati wa kushangilia alivua jezi na kubaki kufua wazi kitu kilichosababisha kuoneshwa kadi ya njano.
Baadaye alioneshwa kadi ya pili ya njano na refa Ricardo de Burgos aliyemwona kama amejiangusha kwa udanganyifu kwa lengo la kumshawishi atoe penalti, Ronaldo kuona hivyo alimfuata na kumsukuma kidogo.
Baada ya kuitupa rufaa hiyo, TAD imeandika "Kumsukuma refa kumeonekana katika picha za mchezo".
Baada ya rufaa ya Ronaldo kushindwa hatacheza katika katika mechi zijazo za Madrid kwenye LaLiga dhidi ya Valencia, Levante na Real Sociedad.
Madrid ilitwaa ubingwa wa Supercopa kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu na kushinda mabao 3-0 ugenini dhidi ya Deportivo La Coruna huku Ronaldo akiwa hayupo.

Comments
Post a Comment