Skip to main content

Ronaldo afungiwa mechi tano, akomaa kupasha na wenzie




MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amefanya mazoezi na wenzie pamoja na kwamba Shirikisho la Mpira wa Miguu Hispania limemfungia mechi tano kutokana na kosa la kumsukuma refa baada ya kuoneshwa kadi ya njano ya pili katika mchezo dhidi ya Barcelona .

Ameweka picha yake akiwa na wachezaji wenzie wa Instagram na kuandika maneno, 'Madrid timu ya ushindi.'

Katika mchezo huo wa kuwania Kombe la Hispania linalowaniwa na bingwa wa La Liga na Copa del Ray, Madrid ilishinda mabao 3-1, mchezo wa marudio utachezwa Jumatano hii katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Barcelona ilipata kipigo cha mabao  3-1 huku ikiwa haina Neymar ambaye amehamia katika timu ya PSG.

Pia Messi na wachezaji wenzie wamerudi mazoezini leo wakijaribu kusahau kipigo walichopata, aliweka picha yao kwenye
Instagram,  na kulaumu kipigo walichopata akisema kuwa ni kibaya, lakini maisha yazima yaendelee. Ndiyom kwanza yanaanza.

Ronaldo amefungiwa mechi tano la Ligi Kuu ya Hispania kutokana na kumsukuma refa baada ya kuoneshwa kadi ya njano ya pili kwa kile alichokiona kama alidanganya kwa kujiangusha katika eneo la penalti alipokuwa akikabana na Samuel Umtiti.

Pia ametozwa faini ya pauni 2,700 (zaidi ya sh. milioni 7.8 kwa tukio hilo la kumsukuma refa Ricardo de Burgos Bergoetxea .

"Kuvuta, kusukuma au kutingisha ya kufanya shambulio lolote dhidi ya wasimamizi wa mechi, hata kama ni ni vurugu ndogo bila ya kusababisha vurumai, itatolewa adhabu ya kufungiwa mechi kuanzia nne hadi 12," inasema kanuni kifungu cha 96.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...