![]() |
| Ibrahim Mussa a.k.a. Roma Mkatoliki |
Mwandishi wetu
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kutoa wimbo mwanamuziki, Ibrahim Mussa maarufu kama, Roma Mkatoliki ametoa na wimbo wa mpya wa Zimbabwe ambao una mashairi yanayozungumzi mambo mbalimbali ikiwemo tukio la kutekwa kwake lilitokea mwanzoni mwa Aprili mwaka huu.
Katika wimbo huo kama zilivyo nyimbo zake nyingine, Roma amehusisha maneno kutoka katika biblia, pia akizungumzia tukio la kutekwa nyara na wajeda ambao hawajui kama walifanya hivyo wenyewe au kutumwa, akiteswa na kufungwa mikono nyuma kwa siku tatu, akiwa amefungwa kitambaa usoni na mikono nyuma, hajui mchana wala usiku na kuhoji ripoti ya tume iliyofanya uchunguzi iko wapi.
Kupitia kwa wimbo huo angalau nyota huyo anayeimba nyimbo za hiphop za harakati amewaeleza mashabiki ni akina nani walimteka na kitu gani walimfanyia, kitu ambacho hakufanya wakati alipopatikana.
Katika wimbo huo amezungumzia mbunge mmoja alisema bungeni kuwa amemtukana rais.
Pia rapa huyo amezungumzia kupatikana kwake ambako kuanza kwa kutabiriwa na ikawa hivyo.
Wimbo huo umekuwa ikipigwa kwenye vituo vya redio, kwenye magari na waendesha bodaboda kuonesha kuwa umepokewa vizuri na mashabiki.

Comments
Post a Comment