Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania Anthony Mtaka, amepongeza mwanariadha, Alphonce Simbu kwa kutwaa medali ya shaba katika mbio za marathoni mashindano ya ya Dunia yanayofanyika London Uingereza.
Katika mbio zilizofanyika jana, Simbu nusura angetwaa medali ya fedha kama si kuzidiwa kwa sekunde mbili na mshindi wa pili Temirat Tora wa Ethiopia, akitumia saa 2:09:51 huku mshindi wa kwanza akiwa Mkenya Geoffrey Kipkorir Kirui aliyetumia muda wa saa 2:08:27.
Akizungumza kutoka Geita, Mtaka alipongeza Simbo ambaye ni bingwa wa mbio za mumbai na mshindi wa tano katika mashindano ya Olimpiki yaliofanyika Rio De Janeiro Brazil na kusema ametimiza maneno yake aliyoahidi wakati akiondoka kuwa hatawaangusha watanzania.
Alisema ushindi huo ni zawadi kwa Rais John Magufuli, na watanzania ambao walikuwa wakiitamani kuona wachezaji wao wanafanya vizuri.

Comments
Post a Comment