Mwandishi wetu
RAIS wa awamu ya pili wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa atakuwa mgeni rasmi katika mbio na matembezi ya Rotary Dar Marathon yatakayofanyika Oktoba 14 (siku ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa awamu ya kwanza Julius Nyerere), mwaka huu Dar es Salaam.
Akizungumza leo mjini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mbio na matembezi hayo, Mwenyekiti na mratibu wa Rotary kwa kushirikiana na Bank M, Catherinerose Barretto amesema mbio na matembezi hayo yatatumika kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika hospital ya CCBRT iliyopo Dar es Salaam
Hopitali ya CCBRT huhudumia watoto wenye matatizo mbalimbali ya ulemavu, wanachangisha fedha ili ili kuiwezesha hosptali hiyo kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.
“Tunayo furaha kubwa kuzindua na kusaini mkataba wa kushirikiana na Bank M kama mdhamini mkuu wa matembezi ya mwaka huu, kuna mambo mapya yameongezeka katika ushiriki wa matembezi ya mwaka huu, kwa mara ya kwanza tutakuwa na Marathon iliyokamilika ya kilomita 42.2.
Alisema katika mbili za mwaka huu wataongeza urefu wa mzunguko kwa waendesha baiskeli na kuwa kilomita 42.2 badala ya km 21 za awali.
Naye Mkurugenzi wa Bank M, Jacqueline Woiso amesema Benki yao itaendelea kushitikiana na Rotary Marathon ambao ni washirika wao katika mambom mbalimbali ya kijamii na maendeleo kwa ujumla.
Katika kuchangisha fesha wakubwa watalipia sh. 35,000 na watoto sh. 10,000 na utaratibu wa kununua fomu hizo utatangazwa kwenye vituo mbalimbali.

Comments
Post a Comment