Skip to main content

PSG yahesabu saa kutambulisha Mbappe



Kylian Mbappe

PARIS, Ufaransa
PARIS Saint Germany baada ya kumnasa Neymar Santos, sasa inahesabu saa kupata saini ya Kylian Mbappe kwa ada ya pauni milioni160 (zaidi ya sh. bilioni 464.7).

Real Madrid nayo imekuwa ikimtaka mshambulkiaji huyo kinda mwenye umri wa miaka 18 wa timu ya Monaco na timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kung'ara katika msimu uliopita .


Lakini timu ya PSG inayomilikiwa na mfanyabiashara raia wa Qatari ndiyo inaonekana kushinda vita, wachezaji wa timu hiyo wameambiwa kuwa Mbappe anajiandaa kutambulishwa katika Uwanja wa Parc des Princes kabla ya Jumatatu.

Kama uhamisho huo utakamilika, PSG itakuwa imewanyakua wachezaji wawili kwa pauni milioni 360 (zaidi ya sh. trilioni moja), wakati ikitaka kuwa moja ya klabu kubwa za Ulaya .

Monaco imekuwa  ikisema inataka kubakia na mchezaji huyo licha ya kutakiwa na Real.

Lakini baba yake  Mbappe anatumaini Monaco itamruhusu mwanaye kuondoka katika majira haya ya joto badala ya kusubiri ipite miezi 12.

Kauli hiyo imewasha taa ya kijani PSG kuanza kufanya mazungumzo kuhusu uhamisho utakaohusisha fedha nyingi kwa mshambuliaji huyo, ina matumaini ya kukubaliana na kuwa iko tayari kutoa dau ambalo linafanana ofa ya Madrid.
Neymar Santos

Mbappe ameshawishika kuhamia PSG baada ya kukutana na kocha wa timu hiyo, Unai Emery aliyemwambia atakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza msimu huu, pamoja na  wamemsaini  Neymar kutoka Nou Camp kwa da ya pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 575).

PSG baada ya kumsaini Neymar kwa kuvunja mkataba wake kutoka Barcelona ilizua swali kama timu hiyo inafuata sheria ya Financial Fair Play ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) inayozitaka kutumia fedha kadiri inavyopata kwa kuuza wachezaji na si kutoka nje.

Uefa ilianzisha sheria hiyo mwaka, 2013 ikilenga kuzisaidia klabu kuepuka kuwa na madeni makubwa kwa kukopa fedha ili kuzitumia kwa kusajili na kuzuia wamiliki kuongezea fedha kwa klabu zao kwa ajili hiyo.

Katika msimu huu tayari PSG inaonekana inaweza kutumia pauni milioni 372.5, pia imem saini beki wa kushoto wa hispania, Yuri Berchiche (pauni milioni14.5)  na raia wa Brazil  anacheza beki ya kulia Dani Alves (bure) .

Real, kwa kumkosa Mbappe anayelipwa pauni 200,000 (zaidi ya sh. milioni 500) kwa wiki, ni pigo kwake na inaweza kufanya kuelekeza nguvu kwa mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...