Mwandishi wetu, Ifakara
SHABIKI wa Simba, Pastory Tulia mkazi wa kijiji cha Sakamaganga amefariki Dunia baada ya mchezaji wa Simba Mohammed Hussein Tshabalala kukosa penalti katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Sakamaganga, Kata ya Ziginali- Ifakara , Omary Siame Omary alisema tukio hilo lilitokea juzi wakati ilipokuwa ikipigwa mikwaju ya penalti kwenye mchezo huo, Tshabalala mchezaji Bora wa Ligi Kuu msimu wa 2016-17 na wa Klabu ya Simba alipokosa mkwaju ambao kama ungeingia lingekuwa bao la ushindi shabiki huyo kwa mshituko alianguka, akapoteza fahamu huku wenzie wakiwa hawajui.
Shuhuda aliyekuwa katika banda la Daniel Kambaga lililokuwa likionesha mpira huo (hakutaka kutajwa Jina), alisema marehemu ni shabiki wa Simba. kabla hakuwahi kuwaambia kwua anaumwa na kabla ya tukio hilo walikuwa wakifutilia mpita kwenye runinga na kushangilia pale wachezaji wa Simba walipokwua wakishangilia
Mazishi ya shabiki huyo yalifanyika jana saa 10 jioni katika kijiji cha Sakamaganga.
Comments
Post a Comment