Skip to main content

Paulinho ampa Mercedes dereva mchina



 Paulinho 

BEIJING, China


MCHEZAJI José Paulo Bezerra Maciel Júnior maarufu kama Paulinho ameonesha kuwa shujaa wa ndani na nje ya uwanja alipokuwa katika Ligi Kuu ya China, kwa mujibu wa mfanyakazi wa Guanzhou

Kiungo huyo wa Brazil hivi karibu amefanya kitendo cha huruma kwa kumpatia dereva wake gari aina ya Mercedes na na vitu vingine kabla ya kuhamia Barcelona  kwa ada ya pauni milioni
36.5, zaidi ya sh. bilioni 105.

Baada ya Paulinho kuondoka katika timu ya Evergrande, Liang Ke ambaye ni mfanyakazi wa klabu ya China aliyokuwa akiichezea, alitumia mtandao wa kijamii unaofanya kazi kama Facebook , Weibo kuonesha ukarimu wake.

Aliandika Paulinho alikuwa mcheshi akimsalimia kila mtu anayekutana naye sehemu ya kazi na kusaidia wengine wenye uhitaji.

'' Ni mtu asiyetaka kupokea fedha yoyote, badala yake anapenda kutoa, kwa mfano alitoa visikilizio vya redio vya kichwani(Beats headphones) na gari lake aina ya (Mercedes-Benz) kwa aliyekuwea dereva wake China.

Alisema hali ya kuwa na roho nzuri si kwamba imetokana na fedha nyingi alizokuwa akipata kwa mshahara wake mkubwa. Kuna watu wengi ambao ni tajiri kuliko Paulinho, lakini ni wachache ni wakarimu na wanaoweza kuwa upendo kama yeye.”

Liang ameelezea jinsi gani Paulinho alivyomleta daktari wa viungo kutoka Brazil ili aje kumtibia na kufanya ajisikie vizuri.

Alisema Paulinho alilipa ada ya tuisheni kwa mtoto wa daktari wa viungo baada ya kumwezesha kusoma katika shule ya kimataifa. Pia alilipia gharama matibabu za mtoto mmoja aliyefanyiwa upasuaji.

“Paulinho aliweza hata kulipia tiketi za ndege na malazi katika hoteli ya nyota tano kwa mtaalamu wake wa viungo na familia yake walipokuwa na mechi za ugenini,'' aliandika.

Mwisho Liang alieleza jinsi Paulinho alivyovaa beji iliyokuwa na maandishi ya ‘FORÇA CHAPE’ na rangi za jezi ya Chapecoense kwa siri kuonesha kusikitika kutokana ajali ya ndege ilitokea na kuua wacheza 19 wa timu hiyo kati ya abiria 71 Novemba mwaka jana nchini Colombia.

Alifanya hivyo baada ya kuomba kwa wasimamizi wa mechi na kukataliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...