Skip to main content

Niyonzima, Okwi gumzo Simba Day leo



WAKATI maadhinisho ya Tamasha la Simba yakifanyika leo, wachezaji Haruna Niyonzima na  Emmanuel Okwi wamekuwa gumzo, kwa mashabiki na wengi wakitaka kwenda uwanjani kuwaona wakati wa utambulisho au watakavyokuwa wakicheza dhidi ya Rayon Spots ya Rwanda  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo utaanza saa 10 ikiwa ni baada ya kupambw ana matukio mbalimbali ya burudani  ambayo yamepangwa  kufanyika.

Katika tamasha la leo, Simba inayonolewa na Kocha, Mkuu Mcameroon Joseph Omog itatambulisha wachezaji wake wapya na wa zamani, pamoija najezi zitakazotumia na timu na mashabiki kwa msimu wa 2017-18.

'Mimi ni shabiki wa Yanga, lakini nitakwenda uwanja kumwona Niyonzima ambaye kuondoka kwake Jangwani kumeniuma lakini ninampenda kwa kuwa ni mchezaji mzuri,'' alisema Juma Hussein ambaye Mkazi wa Kimara.

''Mimi nitanunua jezi nyenye jina la Haruna Niyonzima kwa bei yoyote, kisha nitakwenda uwanjani kumwona na wachezaji wengine waliosajiliwa Simba akiwemo Okwi,'' alisema  Peter Chaula mkazi wa Kinondoni.

Pia ashabiki wengi Dar es Salaam walionekana kwenye meza za kuuza magazeti na kutembelea mitandao kuona habari za Tamasha la Simba, huku katika mazungumza wengi walikuwa wakimzungumzia Niyonzima ambaye alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari jana na leo atakuwepo Uwanja wa Taifa akiwa amevalia jezi za Simba kwa mara ya kwanza tangu alijiunge akitokea kwa mahasimu wao Yanga alikocheza kwa misimu sita akitoke APR ya Rwanda.

Kwa upande wa mchezaji mpya kutoka klabu ya Yanga, Haruna Niyonzima alisema  hana maneno mengi mguu ndi utaongea.

"Sina maneno mengi kikubwa ni ushirikiano na mguu ndiyo utaongea, hivyo wapenzi waje kwa wingi kuangalia nini tunafanya wachezaji wao, "alisema Niyonzima.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Msaidizi wa klabu hiyo, Jackson Mayanja, alisema utakuwa wa tatu kwa kikosi chao ambacho kilicheza mechi mbili nchini Afrika Kusini.

Alisema kupitia mchezo huo wataangalia wachezaji wao wapya na wa zamani  ikiwa ni shehemu ya maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu huo.

"Tuna amini mchezo huu dhidi ya Rayon utatupa sura ya kikosi chezo kabla ya kuanza kwa msimu, tutatumia zaidi kuangalia kitu gani kinatakiwa kufanyika kabla ya msimu mya haujaanza,"alisema Mayanja.



Ciao...

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...