![]() |
| Haji Manara akimtambulisha, Haruna Niyonzima Dar es Salaam jana. |
HAYAWI hayawi hatimaye yamekua. Kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima amevaa kwa mara ya kwanza nyuzi (jezi) zenye rangi nyekundu na nyeupe za klabu yake mpya ya Simba na kupasha na wachezaji wenzie leo.
Picha ya nyota huyo akiwa jezi hiyo imetoka kwa mara ya kwanza na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, huku wa mashabiki wa simba wakiipamba na maneno ya kumsifu na kuwaponda watani zao Yanga.
Niyonzima aliyeichezea Yanga kwa misimu sita mfululizo baada ya kuhamia kutoka Rwanda anatarajiwa kutambulishwa na wachezaji wenzie kesho Uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Simba.
Niyonzima ametua Simba baada ya Yanga kushindwa kuelewana naye baada ya mkataba wake kwisha.

Comments
Post a Comment