![]() |
| Ngao ya jamii ambayo ilikuwa imekosewa kuandikwa neno SHEILD badala ya SHIELD. |
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya marekebisho katika maneno yaliondikwa kwa kukosewa katika Ngao ya Jamii ambayo ilikabidhiwa kwa Simba baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 5-4 kwenye mchezo uliofanyika Jumatano iliyopita
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
TFF iliomba radhi na kuahidi kutoa Ngao ya Jamii nyingine na sasa itakabidhiwa kwa Simba kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC jijini Dar es Salaam.

Comments
Post a Comment