PARIS, Ufaransa
MWANASOKA ghari zaidi duniani , Mbrazil Neymar Santos (25) amewasili katika mji mkuu wa Ufaransa , Paris kujiunga na timu ya Paris Saint-Germain akitokea Barcelona ya Hispania.
Awali mashabiki wengi walijitokeza kwenye duka la vifaa la PSG, Champs Elysees kununua jezi ya yenye jina la Neymar na namba 10 mgongoni, kisha kumlaki baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Le Bourget kwa ndege ya kukodi.
Neymar, kwa ada iliyoweka rekodi mpya ya usajili ya pauni 200 (zaidi ya sh. bilioni 589) akitokea Barcelona ya Uhispania, amesaini mkataba wa miaka mitano.
![]() |
| Mashabiki wa timu ya PSG wakiwa wamepanga foleni kwenye duka la timu ya PSG kwa ajili ya kununua jezi yenye jina Neymar kabla ya kuwasili kwenye klabu yao jana. |



Comments
Post a Comment