![]() |
| Neymar akishangilia kwa kuonesha msuli alipofunga mabao mawili katika timu ya PSG jana. |
PARIS, Ufaransa
NEYMAR Santos ametoa maneno yanayoonekana kama ameushambulia wakurugenzi wake wa zamani katika timu ya Barcelona kwa kusema timu hiyo inastahili kuwa vizuri zaidi.
Akizungumza baada ya mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi cha PSG iliyopambana na Toulouse na kushinda mabao 6-2, Neymar alisema kuna watu (wakurugenzi) ambao wako katika uongozi ambao hawastahili, kwa mwelekeo wa Barca.
''Ninataka kusema ukweli ninawasikitikia sana,nimekaa kwa miaka minne pale na nilikuwa na furaha sana. Mwanzoni nilikuwa na furaha. Nimetumia miaka minne vizuri pale na nimeondoka nikiwa na furaha. Lakini wao (wakurugenzi wa klabu), Hapana. Kwangu mimi si watu wanaotakiwa kuwa pale kwa mwelekeo wa Barca," alisema Neymar.
Pamoja na kupata fedha nyingi kwa ada ya Neymar, Barcelona imeshindwa kupata mchezaji wa kuziba pengo yake.
Barce imetuma ofa tatu kwa Livepool ya mwisho ikiwa ya zaidi ya euro milioni 100 kumsaini Philippe Coutinho, lakini imekataliwa, pia ilitaka kumsaini mchezaji wa Dortmund, Ousmane Dembele na imeshindwa.
Timu hiyo imekuwa ikikosolewa kwa kutumia euro milioni 40 kumsaini Paulinho, ambaye amecheza katika Ligi Kuu ya China mwa miaka miwili kwenye timu ya Guangzhou Evergrande.
Hata hivyo Neymar amesema kuwa hawezi kutoa maoni kuhusu kilichofanyika katika klabu hiyo kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa mwishoni mwa mwezi huu.
"Siwezi kusema kwa sasa niko katika timu nyingine. sijui kinachoendelea pake, lakini ninawaona wachezaji wenzangu wa zamani wakiwa hawana furaha, kitu hicho kinanifanya niwe na huzuni," alisema na kuongeza kuwa anatarajia mambo yatakaa vizuri na kuwa kama zamani ambapo ilikuwa timu tishio.

Comments
Post a Comment