![]() |
| Neymar Santos |
PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Paris Saint Germany, Neymar ameishitaki klabu yake ya zamani ya Barcelona katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) akidai haijamlipa kiasi cha pauni milioni 23.97 (zaidi ya sh. bilioni 68.5) zinazotokana na bonasi na mkataba aliousaini Novemba mwaka jana..
Amechukua hatua hiyo baada ya Barcelona kusema itamshitaki na kutaka arudishe fedha kiasi cha pauni milioni 7.8 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 22.3 ilizompatia kama bonasi baada ya kuongeza mkataba wa miaka mitano.
Fifa limesema kuwa ni kweli imepata madai ya Neymar dhidi ya Barcelona.
Jumanne iliyopita, Neymar alisema ataichukulia hatu za kisheria klabu hiyo ya Catalan. Utawala wa mchesaji huyo Group N & N Consultoria imesema kuwa alitimiza kila kitu kinatakiwa katika mkataba wake
Timu ya PSG ilivunja rekodi ya usajili kwa kumsaini neymar kwa ada ya pauni milioni 200, ikiwa ni kiasi cha fedha kilichowekwa kwenyekipengere cha mkataba wake, ili kuuvunja au kumnunua.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, ameisaidia kutwaa kombe la La Liga mara mbili, Copas del Rey vikombe vitatu na kutwaa taji la Ligi ya mabingwa 2015 katika kipindi cha miaka minne aliyokuwa Barcelona.

Comments
Post a Comment