Skip to main content

Neymar ahesabu saa kutua PSG kwa bil 586/-






MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Neymar Santos sasa inaonekana anahesebu saa kutua katika timu ya Paris St-Germain, baada ya kupewa ruhusa kwenda kufanya mazungumza na timu ya Paris St-Germain kuhusu uhamisho wake utakaovuja rekodi ya dunia kwa ada ya pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 586).

Mchezaji huyo leo amewaambia wachezaji wenzie walipokuwa mazoezini kwamba ametakiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Hispania.

Amepewa ruhusa na kocha wa Barca kocha Ernesto Valverde kutofanya mazoezi na kuangalia namba ya kushughulikia hatima yake ya baadaye.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 kwenye mkataba wake kuna kingele cha kuuvunja kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 586), kiasi ambacho PSG inadaiwa iko tayari kulipa.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa miamba hiyo ya La Liga, Javier Tebas katika mahojiano yake na Mundo Deportivo kusema watawachukulia hatua mabingwa wa zamani wa Ufaransa kwa kuwashtaki Fifa kama Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ulaya halitachukua hatua.

Pia Rais wa PSG , Nasser Al-Khelaifi anajua kuhusa dhamira ya Barcelona.

Neymar alihamia Barcelona akitokea timu ya Santos ya Brazil mwaka 2013 kwa ada ya pauni milioni 48.6 (zaidi ya sh. bilioni 144) na kusaini mkataba wa miaka mitano mwaka 2016.

Wakala wake Wagner Ribeiro leo ameandika kwenye Twitter akiwa Paris,  alisema mwaka jana mteja wake alipewa ofa ya kulipwa mshahara wa pauni  650,000 (zaidi ya sh, bilioni 1.9) bila ya kutosha kodi.

Pia alisehe nyota huyo ilibaki kidogo ajiunge na Manchester United.

Neymar amefunga mabao 105 tangu atue Barcelona, ameisaidia kutwaa makombe mawili ya Ligi Kuu vikombe vitatu vya Copas del Rey na Ligi ya Mabingwa.


Timu ya PSG inamilikiwa na kampuni ya Qatari Sports Investment (QSI) inayofanya biashara gesi asili ina jeuri ya fedha .

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...