TIMU za Napoli, Sevilla na Celtic zimefuzu hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa baada ya kushinda mechi za marudiano za mchujo zilizopigwa usiku wa kuamkia leo.
Mabao ya Napoli dhidi ya Nice ya Ufaransa yalifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Jose Callejon (dk 48) na Lorenzo (dk 89) na kusonga mbele kwa uwiano wa mabao 4-0 baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa awali.
Sevilla imesonga mbele kwa uwiano wa mabao 4-3 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa jana dhidi ya Istanbul Basaksehir.
Celtic bila ya kutarajiwa imepata kipigo cha mabao 4-3 dhidi ya Astana mjini Kazakhstan lakini imesonga mbele kwa uwiano wa mabao 8-4, baada ya awali kushinda mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza. Celtic imesonga mbele kwa mara ya pili mfululizo.
Pia timu ya Olympiakos nayo imesonga mbele katika hatua ya makundi baada ya kushinda bao1-0 ugenini dhidi ya Rijeka. Olympiakos imesonga mbele wa uwiano wa mabao 3-1.
Pia timu ya Maribor imesonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Hapoel Be'er Sheva. Matokeo hayo yamefanya timu hizo kufungana mabao 2-2, katika mchezo wa awali mabingwa hao wa Slovenia walishinda mabao 2-1 ugenini.
Timu zilizoshindwa katiak mchuzo baada ya mechi za jana, Nice, Istanbul Basaksehir, Astana, Rijeka na Hapoel Be'er .

Comments
Post a Comment