Skip to main content

Mwakyembe awataka wajumbe kutokosea kuchagua viongozi TFF


Dk. Harrison Mwakyembe

Mwandishi wetu

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wana dhamana kubwa ya kuchagua viongozi wazuri watakaosaidia kuleta maendeleo ya soka nchini.

Akizungumza wakati uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi mjini Dodoma leo, Mwakyembe amesema macho yote ya watanzania wapenda  soka yameelekezwa kwa wajumbe wa 128 kutekeleza kazi kubwa ya katiba yao.

Mkutano huo utamchagua Rais wa Shirikisho, Makamu na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji ya TFF watakaohudumia kwa miaka minne.

Amesema kama ilivyo kawaida ya chaguzi zote presha huwepo si tu kwa wagombea, pia kwa wapigakura lakini kwa nia njema ya kupata viongozi bora wa kuendesha chombo adhimu kwa ajili ya maendeleo ya soka nchini.

'' Ndugu wajumbe viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema, wasioyumbisha na vishawishi vya mpito, wanaongozwa na uzalendo.''

''Serikali inaamini katika mkutano huu kuna wajumbe makini wasioyumbishwa na vishawishi, wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo wa hali ya juu ambao wataibua viongozi bora wa TFF wenye ari, moyo, uelewa weledi na  uadilifu unaotakiwa utakaosaidia kuipeleka soka katika hatua ya mbele,'' amesema Waziri Mwakyembe.

Amesema mafanikio huwa hayaji kwa maneno, kukamia bila ya kuwekeza na kujenga mazingira stahili, watanzania wanajua kuwa mpira ni mazoezi,  ni nidhamu, ni afya, na ni ajira ya nguvu.

Mazingira hutengenezwa na vuiongozi makini tu wanaotambua thawabu ya uwajibikaji na kuheshinmu katiba, iliyowaingiza madarakani, wanaothamani uongozi wa pamoja.

Amesema kwa mara ya kwanza viongozi watakaochaguliwa wataapishwa mbele ya wapiga kura, kufuata sheria na kanuni kama vilivyo, wataapa kiapo cha utii mbele ya msajili.

Amesema kwenye mkutano huo kuna ugeni kutoka CAF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika) na Fifa) Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu), wajumbe wanatakiwa  kuwaonesha kwa vitendo  ukomavu wa kidemokrasia wa Tanzania katika uchaguzi duniani.

Amesema imepita miaka mingi hadi mwaka huu Tanzania imeshirikia mashindano ya Afcon kwa vijana umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys. Pia mwaka huu Tanzania imefanya vizuri katika mashindano ya Cosafa kwa kushika nafasi ya tatu.

Amesema Tanzania inataka viongozi watakaolipeleka taifa mbali zaidi kimaendeleo, watakailea timu ya Serengeti Boys ambayo imepanda na kuwa ya chini ya umri wa miaka 21 Ngorongoro Boys ili kushiriki olipiki ya mwaka 2020 inatumia wachezaji wenye umri wa mika chini ya 23.

Wanatakiwa  viongozi watakaoshirikiana na serikali kwa karibu kufanya maandalizi mazuri  ya mashindano ya Afcon kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yanakaofanya mwaka 2019 nchini Tanzania kama wenyeji.

Amesema wanatakiwa viongozi watakaochaguliwa leo kuanza kazi mara moja ya kuiandaa timu ya Serengeti Boys mpya inayotoka na vijana walkiopatikana miaka miwi,li ilipita kwenye mashindano ya watoto wa chini ya miaka 13 ambao wamekusanywa na kuwekwa kwenye moja ya vituo michezo nchini.

Wanatakiwa viongozi ambao watashirikina na serikali kuwalea watoto wenye vipaji vya soka walioibuliwa kwenye mashindano ya karibuni  ya Umisseta na Umitashumta yaliofanyika hivi karibuni.

'' Tunataka uongozi ambao unatambua na kusimamia kanuni ya Fifa ya Club Licensing kwa kujiamini kwani huo ni msingi wa mafanikio ya soka nchini.

''Serikali inataka uongozi ambao unatambua kuwa Fifa haikubatii rushwa, unatambua kwamba CAF haikumbatii rushwa na wala ubadhirifu kama ambavyo serikali haikubatii rushwa na ubadhirifu,'' amesema.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...