Skip to main content

Mwakyembe ataka wanariadha kurudi na medali London








Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe (watatu kulia) akimkabidhia bendera  ya Taifa nahodha wa timu ya Taifa  ya Riadha, Alphonce Simbu  iliyoangwa Dar es Salaam jana kwenda London, Uingereza kushiriki mashindano dunia ya riadha yanayotarajiwa kuanza Ijumaa wiki hii.


Mwandishi wetu
TIMU ya taifa ya mchezo wa riadha imeagwa rasmina kukabidhiwa bendera ya taifa kabla ya safari ya ya kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yanatotarajiwa kufanyika London, Uingereza kuanzia Agosti 4 mwaka huu.


Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji nane ilikabidhiwa bendera ya taifa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mwakyembe alisema wizara serikali  iko bega kwa bega na wadau wa michezo hapa nchini katika kuhakikisha kuwa sekta hiyo inapiga hatua.

“Kwanza kabisa nimetiwa moyo sana na ari ya vijana waliyonayo na kama mlivyoona na kusikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari, vijana hawa wamepikwa vizuri na wana ari, moyo na uzalendo mkubwa na kilicho mbele yao ni kitu kimoja tu, kupambana kufa na kupona na kurudi na medali” alisema Waziri Mwakyembe.

“Tumeshazijua siri za wenzetu kufanikiwa katika riadha, mazoezi ndiyo kila kitu hata uvae hirizi ama utumie madawa huwezi kufanikiwa”.

“Unaposhinda medali unapandishiwa bendera na kupigiwa wimbo wa taifa hiyo ni heshima kubwa, vijana wangu tukimbie hata miguu ikifika kisogoni kimbieni”.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka alisema mbali na jitihada kubwa zinazofanywa na chama hicho  zipo changamoto nyingi ambazo zinahitaji nguvu za pamoja ili kuhakikisha kuwa riadha inaendelea mbele.

Amesema kuwa kwa kutambua hilo na kwa kutambua umuhimu wa wadau mbalimbali, wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu sana na wadhamini (DStv) na majeshi mbalimbali kama vile JKT na JW ambapo wanariadha wengi wanatoka.


Jumla ya wanariadha wataoshiriki mbio ndefu za kilomita 42 ni, Alphonce Simbu mwenye rekodi ya 2:09.10 aliyo iweka hivi karibuni katika mashindano ya London Marathon, Ezekiel Jafari Ng’imba 2:11.55 aliyoiweka katika mashindano ya Hannover Marathon mwaka 2017.

Wengine ni Stephano Huche Gwandu 2:14.18 mashindano ya Tunis Marathon, Sara Ramadhani Mkera 2:33.08 akishinda katika mashindano ya Dusseldorf mwaka 2017 na Magdalena Crispin Shauri 2:33.28 akishinda katika mashindano ya Hamburg Marathon mwaka 2017.

Washiriki watatu waliosalia watakaoshiriki mbio fupi ni, Gerald Geay meta 5,000, Emmanuel Ginki Gisamoda meta 5,000 na Failuna Abdi Matanga akishiriki mbio za meta 10,000.

Mashindano ya dunia ya riadha yanatarajiwa kuanza Agosti 4 kuisha Agosti 13, mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...