Mwandishi wetu
MSANII mkali wa muziki wa kughani wa asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto ametoa wimbo mpya aliouopa jina la Kitendawili ambao ameshirikishi msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mkali kuimba nyimbo za mahaba, Kassim Mganga.
Wimbo huo uliotayarishwa na mtozi Man Walter umeachiwa mwanzoni rasmi jana, kama zilivyo nyimbo zake nyingine, Mpoto ameweka mafumbo akianza na maneno kitendawili tega, kuku anayetaga hachinjwi, akichinjwa kuna msiba.
Anazungumzia mambo mbalimbali wanayokutana nayo wananchi na uongozi. Wimbo huo umeanza kuwabamba mashabiki wa muziki wake.

Comments
Post a Comment