Jose Mourinho akiwa na Antonio Conte.
LONDON, Uingereza
|
Awali kocha Conte alilalamika kutokana na ku timu yake kumuuza Nemanja Matic kwa mahasimu wao Manchester United.
Lakini Mourinho alisema: “Wakati unapouza na kuendelea kununua, kisha hapo kuna tatizo gani? Pengine unakuwa imara.
“ Tatizo ni kama unauza huku hununui. Watu wanasema Chelsea imepoteza kiungo muhimu. Lakini unapoteza mmoja na kisha unanunua Bakayoko na Drinkwater kwa mfano, kuna tatizo gani?”
Conte ametumia pauni milioni 58 (zaidi ya sh. bilioni 166) kwa kumsiani mchezaji nyota wa Hispania, Alvaro Morata na pauni milioni 31( zaidi ya sh. bilioni 89) kwa mlinzi wa kijerumani, Antonio Rudiger.
Bado kocha huyo amekuwa akilalamika kwamba anataka wachezaji zaidi ili kuimarisha kikosi chake na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England.
United jana ilicheza na Swansea , Mourinho amempiga kijembe Conte kutojificha katika kisingizio cha soko la uhamisho.
Katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu United ilishinda mabao 4-0 dhidi ya West Ham.
Mourinho amesifu kikosi chake akisema kuwa, kama walikuwa na matatizo yatakwenda kuisha baada ya dirisha la usajili kufungwa. Hawana shida.
United iliipiku Chelsea kumsaini mshambuliaji Romelu Lukaku kutoka timu ya Everton, ilikuwa na matumaini makubwa ya kumpata lakini ilichelewa kupeleka fedha kukuta akielekea Old Trafford.

Comments
Post a Comment