![]() |
| Rais wa Fifa, Gianni Infantino, |
RABAT, Morocco
SHIRISHO la Mpira wa Miguu la Morocco limetangaza nia yakutaka kuandaa michuano ya Kombe la Dunia 2026, likijipa nafasi kubwa ya kuandaa mbele ya Canada, Mexico na Marekani ambayo nazo zinaitaka nafasi hiyo.
Chini ya utaratibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), michuano ya Kombe la Dunia 2026 haiwezi kufanyika Ulaya au Asia na kufanya Afrika, Oceania, Marekani ya Kaskazini au Kusini kuwa sehemu pekee ambazo zinaweza kupata uenyeji huo.
Pamoja na kuwepo taarifa kuwa Chile inataka kuandaa, Canada-Mexico na Marekani zimeomba na kutangazwa Aprili mwaka huu.
Juzi Ijumaa ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho kutuma maombi, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco lilitoa taarifa fupi kukanusha kupinga mambi ya nchi zilizo katika Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu vya Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean (CONCACAF).
Mashindano ya Kombe la Dunia 2026, yatafanyika chini ya utaratibu wa timu 48, baada ya Fifa kuthibitisha muundo mpya Januari.
Afrika imewahi kuandaa michuano ya kombe la Dunia mara moja, nchini Afrika Kusini mwaka 2010, lakini kwa Morocco sasa inaomba kwa mara ya tano.
Mwenyeji wa fainali hizo anatarajiwa kutangazwa Mei 2020.

Comments
Post a Comment