![]() |
| Mo Farah akifurahia kutwaa medali ya dhahabu ya sita katika mbio za Dunia. |
LONDON, Uingereza
BAAADA ya kutetea ubingwa mbio za Dunia meta 10,000, Mo Farah amesema anaamini pamoja kuwa na maumivu ya mguu atashindana ili kutetea ubingwa wake katika mbeo za meta 5,000.
Mo mwenye umri wa miaka 34, aliteleza mara mbili na kutaka kuanguka kabla ya kukaa sawa na kukimbia kwa ushindani na kutwaa ushindi katika mashindano ya riadha ya dunia 2017 yaliofanyika jana katika Uwanja wa London
"Nimeumia mguu wangu na ninakwenda kuonana na daktari wangu," alisema.
Mbio za meta 5,000 zitafanyika kwenye joto kali Jumatano wiki ijayo, kwa Farah inaweza kuwa mbio zake za za mwisho kabla ya kuhamia katika marathon.
"Mguu wangu una shida, nilitaka kuanguka mara mbili na nikajaribu kusimama.
"Nimeumia. Niliamua kujikaza. Nina majeraha na michubuko, ninategemea kupona na kujiandaa na mbio za meta 5,000, kuna muda kidogo wa kujiandaa," alisema Mo.
Katika mashindano hayo Mo alitumia dakika 26:49:51ukiwa ni muda wa kasi zaidi katika mbo za meta 10,000 kuanzia mwaka 2011, alimzidi pungufu ya sekunde moja Mganda Joshua Cheptege aliyeshika nafasi ya pili huku mkenya Paul Tanui akimamata nafasi ya tatu.

Comments
Post a Comment