SIMBA imelazimishwa matokeo ya suluhu dhidi ya Mlandege katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku wa leo.
Mlandege ambayo Jumapili ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, imewakomalia Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho walioweka kambi Unguja kujiandaa kwa mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao hao Jumatano, Agosti 23 mwaka huu.
Mechi za majaribio zinazofanyika kwa sasa zinaitwa na mashabiki za kujaribu mitambo kama inalipua, kwa kutoa suluhu ina maana Mlandege imeidhibiti mitambo ya Simba isilipue.
Matokeo hayo yamewatia wasiwasi mashabiki wa Simba ambao wanaamini wana safu nzuri ya ushambuliaji.
Katika michezo yake mwili ya mwisho Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha Simba kilichocheza ni; Aishi Manula, Ally Shomary, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salim Mbonde, Method Mwanjali, Jonas Mkude/James Kotei , Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla , Mohammed Ibrahim, Laudit Mavugo/Juma Luizio , Haruna Niyonzima na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Jamal Mnyate .
Comments
Post a Comment