Skip to main content

Mkutano wa Simba upo kama kawaida




KLABU ya Simba kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara imetoa taarifa kwamba mkutano mkuu wa klabu uliopangwa kufanyika kesho Agosti, 13 utafanyika kama kawaida na kwa sasa ukifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta, Dar es Salaam, taarifa zaidi isome hapa chini.
Klabu ya Simba inawatangazia Wanachama wake na wadau wa mchezo wa kandanda kote nchini kuwa Mkutano wake mkuu wa kawaida wa kila mwaka upo pale pale. 
Hatua hiyo inafuatia na Hukumu iliyosomwa leo katika Mahakama ya kisutu, kufuatia zuio la kuzuia Mkutano huo, liliowekwa na mmoja wa wadhamini wa klabu Mzee Hamis kilomoni. 

Kikosi cha Simba

Kwenye hukumu hiyo,mahakama hiyo ilitupilia mbali shauri hilo. 
Mkutano huo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 13-8-2017, kuanzia saa Nne kamili asubuhi, ukitanguliwa kwa Wanachama wa klabu kujiandikisha kuanzia saa mbili kamili asubuhi. 
Klabu imeamua kufanyia mkutano huo kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere international Conference Centre). Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha(IFM), Na itakuwa mara ya kwanza kwa vilabu vya michezo nchini kufanyia mkutano wake kwenye kituo hicho kilichobeba jina la Baba wa Taifa hili. 
Uongozi wa Simba unawaomba wanachama wake kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano huo muhimu,huku mahitaji yote muhimu yakipatikana siku hiyo ikiwemo Vinywaji baridi na Chakula cha mchana.
Klabu inawaomba tena Wanachama wake wenye hoja tofauti waje kuzitoa ndani ya Mkutano huo kama inavyoagiza katiba ya klabu. 
Hakika huu ni ushindi mkubwa sio tu kwa klabu, bali kwa Mustakbali mzima wa maendeleo ya mchezo huu murua zaid nchini na kote Ulimwenguni. 

Awali  bodi ya wadhamini ya Simba ambayo ikiongozwa na Hamisi Kilomoni ilifungua kesi ya kupinga mkutano mkuu kwa madai ajenda itakayojadiliwa katika mkutano huo ni klabu hiyo kujiendesha kibiashara kitu ambacho wanaamini mali  za klabu zitamilikiwa na mtu binafsi.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...